CAF yatoa majina 34 ya wachezaji bora barani Africa

Unknown | Thursday, October 11, 2012 | 0 comments

Shirikisho la kandanda barani Afrika, CAF, limetoa orodha ya wachezaji 34 ambao watawania tuzo ya mchezaji bora zaidi wa soka katika bara hilo mwaka 2012.Kati ya wachezaji hao, ni mchezaji Yaya Toure, kutoka Ivory Coast, na ambaye huichezea klabu ya Uingereza ya Manchester City.
Toure alitangazwa mshindi wa tuzo hiyo mwaka uliopita.
Katika orodha hiyo, wamo wachezaji watatu ambao huvichezea vilabu vya Afrika.
Wachezaji wawili wa Zambia, Rainford Kalaba na Stoppila Sunzu, wote ni wachezaji wa klabu ya TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, na Youssef Msakni kutoka Tunisia ni mchezaji wa Esperance.
Msakni hata hivyo anatazamiwa kuihama Esperance, na kuelekea Qatar mwezi Januari mwaka ujao, kujiunga na klabu ya Lekhwiya.

Kalaba na Sunzu tayari wana sifa za kutosha, baada ya kuwa miongoni mwa wachezaji walioiwezesha Zambia kuibuka mabingwa katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu nchini Gabon.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments