Man City, Arsenal zashinda

damas venance | Sunday, October 28, 2012 | 0 comments

Katika Ligi ya Premier ya England timu maarufu za Manchester City na Arsenal zimenusurika baada ya kupata ushindi katika mechi za Jumamosi ya jana.
Katika mechi iliyochezewa nyumbani ugani Etihad,  Muajentina Carlos Tevez alipachika bao wavuni kunako dakika ya 61 na hivyo kuipatia timu yake ushindi muhimu dhidi ya Swansea City.
Mechi hiyo ilikuwa na dakika 12 sekunde 42 za nyongoza na hivyo kuvunja rekodi ya muda wa ziada wa kipindi cha pili katika historia ya Ligi ya Premier.
Katika upande mwingine, Arsenal imenusurik
a kwa kuifunga timu inayoshika mkia ya Queens Park Rangers katika mechi iliyochezewa uwanja wa Emirates mjini London. Mkwaju wa  Mikel Areta katika dakika ya 84 ndio uliowanusuru vijana wa Gunners waliokuwa wakicheza nyumbani.
Arsenal walifanikiwa kufunga bao hilo baada ya Queens Park Rangers kubakia na wachezaji 10  pale Mkameroon Stepane Mbia alipopewa kadi nyekundu katika dakika ya 79

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments