KAULI YA WEUSI KUHUSU KUKAMATWA KWA LORD EYEZ
Msemaji wa kundi la Weusi Nikki
wa Pili ametoa kauli ya kwanza toka kukamatwa kwa Lord Eyez wa kundi
hilo kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya gari la Ommy Dimpoz.
Namkariri Nikki wa Pili akisema
“kwanza hiyo ni habari ya ghafla alafu ni ya kusikitisha na kushtua, ni
habari ambayo imetupa shida na mpaka sasa inatupa shida sana kwa sababu
watu wengi wanatupigia simu kutuuliza inakuaje”
“Ukiangalia kwenye mitandao ya
facebook na twitter kote imesambaa, unajua ukijua ukweli ni kitu cha
msingi sana kwa sababu sisi pia tulikua hatufahamu kilichotokea, kwa
hiyo cha kwanza tulichokifanya ni kutaka kujua kilichotokea, mfano mimi
niliona kwenye mitandao kwamba Lord Eyes amekamatwa kwenye eneo la tukio
yupo kwenye gari lakini kufatilia nikaja kugundua haikua eneo la tukio
na sio gari hilo, uhalifu ulifanyika alhamis na alikamatwa jumamosi” –
Nikki wa Pili
Category: celebrity
0 comments