Obama aahidi kuleta maendeleo
Rais
Barack Obama amewahakikishia wamarekani kulisogeza mbele zaidi taifa
hilo baada ya kumbwaga mpinzani wake kutoka chama cha Repablican katika
kinyang'anyiro cha urais wa taifa hilo, Mitt Romney.
Baada ya
kupata fursa ya kuhutubia umma rais Obama alisema kwamba uchaguzi huo wa
watu wa Marekani unawakumubusha kwamba wakati barabara yao imekuwa
ngumu na safari yao pia imekuwa ndefu, tayari wapo safarini, wametafuta
njia na kwamba wanatambua kutoka moyoni mwao kwamba wanajukumu kubwa na
kuahidi kwamba mambo mazuri yanakuja.
"Ninaamini tunaweza kutimiza
misingi ya ahadi tuliyo nayo, la msingi ni kwamba kama unataka kufanya
kazi sana haijalishi wewe ni nani,au unatokea wapi, au unaonekanaje au
wapi unapenda. Haijalishi wewe ni mweusi au mweupe, au Muhispania au
Muasia, au Mmarekani asilia, au kijana au mzee, au tajiri au masikini,
mlemavu au mkamilifu, shoga au mtu wa kawaida unaweza kuleta ushindi
Marekani kama unataka kujaribu". Rais Obama alisema maeneo hayo ya kutia
faraja mbele ya umati mkubwa wa wamarekani akiwa katika mji wake wa
nyumbani huko Chicago.
Obama aahidi kushirikiana na Republican
Akiwa
jukwaani na mke wake na watoto wake Sasha na Maria alirejelea maneno ya
kupigania maisha bora kwa watu wa kipato cha wastani na kutimiza ndoto
ya kuifanya Marekani kuwa taifa lenye tija zaidi. Aidha alisisitiza
kwamba katika kutimiza azma hiyo na hasa kupunguza nakisi,kuleta
mabadiliko katika sheria za uhamiaji na kupunguza hali ya taifa hilo
kutegemea mafuta kutoka nje amesema watashirikiana na viongozi wa
Republican pia.
Romney ampongeza Obama
Kwa
upande wake Romney aliwaambia wafuasi wake kwamba alikuwa akisali wakati
wote ili aweze kushinda nafasi ya urais wa taifa hilo kubwa kabisa
duniani. Akizungumza kabla ya kuungana na mkewe Ann, sambamba na familia
yake na mgombea mwenza Paul Ryan alisema vilevile angalipenda kutimiza
matakwa yao ya kuliongoza taifa hilo katika mwelekeo mpya lakini taifa
limechagua kiongozi mwingine. Kwa hivyo yeye, mke wake pamoja na wafuasi
hao wanaungana kumuombea heri rais Obama na taifa hilo kubwa kwa
ujumla.
Obama anachaguliwa tena kuongeza taifa hilo kwa kipindi
kingine cha miaka menne wakati taifa hilo likikabiliwa na kiwango
kikubwa cha tatizo la ajira la asilimia 7.9. Kumbukumbu zonaonesha
hakuna rais wa Marekani aliengia madarakani kwa awamu ya pili tangu
kumalizika kwa vita vya pili vya dunia kukiwa na kiwango cha tatizo la
ajira cha asilimia 7.2. Ukuaji wa kiwango cha ajira kwa mwaka huu 2012
kimesalia asilimia mbili. Lakini kwa wakati wote rais Obama alikuwa
akiwakumbusha wapiga kura kwamba hali hiyo amerithi baada ya kuchaguliwa
kwake 2008.
Category:
0 comments