Published On: Thu, Oct 4th, 2012 World Wide News | By Damas venance Obama na Romney wapambana kwenye mdahalo
Uchunguzi wa maoni ulofanywa na kituo cha televisheni cha CNN mara tu
baada ya mdahalo, unaonesha kwamba asili mia 67 ya wapiga kura
walohojiwa wanasema Romney alimshinda Obama kwenye mdahalo huo. Huku
asili mia 26 wakisema Obama alifanya vizuri.
Wanasiasa hao wawili kwa sehemu kubwa walizungumzia uchumi, na namna ya kubuni nafasi za ajira na mipango yao ya kodi na afya.
Mitt Romney anasema ni lazima kutafuta njia nyingine ya kubuni ajira
akisema mipango yake ni pamoja na kuongeza uzalishaji nishati, kupanua
biashara ya kimataifa, kubuni nafasi zaidi ya mafunzo ya kazi na kuleta
uwiyanio katika bajeti.
“Ndio tunaweza kuleta mabadiliko, na si kutumia njia tuliyo nayo
sasa ambayo rais anaeleza ni kuongeza kodi kwa matajiri na kupunguza wa
watu wa tabaka la chini. Mimi sitompunguzia mtu kodi kwa wakati huu
mgumu wa uchumi. Mimi nina nukta tano ya mageuzi, kupanua uchimbaji
mafuta na hivyo kupatikana nafasi milioni 4 za ajira, kupanua masoko ya
Amerika Kusini kwa biodhaa ya Marekani, kuadhibu China wanapodanganya,
wamarekani wapate ujuzi unaohitajika kwa kazi na kuhamasisha biashara
ndogo ndogo.” alisema Romney.
Kwa upande wake Obama anasema anakubaliana na Romney kuimarisha
uzalishaji nishati lakini anasema kwa kuangalia namna ya kutumia
teknolojia ya kisasa ya nishati mbadala ya juwa na upepo na kurudisha
nafasi za kazi zilizosafirishwa nje ya nchi.
“Suala hii leo si tulikuwa wapi, bali ni tunakwenda wapi, Romney
anataka kuwapunguzia matajiri kodi na kupunguza usimamizi katika
biashara kubwa. Mimi ninataka kutumia pesa kwa ajili ya elimu na mafunzo
ya kazi, nishati mbadala na kubadili kanuni za kodi. Na kutumia fedha
zinazopatikana kwa kumaliza vita viwili na kutumia kukarabati Marekani,”
alisema rais Obama.
Suala jingine waliozungumza kwa urefu na muhimu ni mpango wa mageuzi
ya huduma ya afya maarufu kwa jina la ‘Obamacare’. Romney anapinga
mpanmgo huo akisema haijabidi kwa serikali kuu kuamrisha watu na
madaktari juu ya kile kilicho bora kwa afya yao.
Anasema inabidi kuachia mashoko na biashara kuendesha huduma za afya.
Obama anapinga wazo hilo akisema huo ni mpango Romney aliupitisha akiwa Gavana wa Massachusetts.
“Ukifutilia mabli mpango huo wa ‘Obamacare’ – jina ambalo
nimeanza kupenda – mara moja wazee watajikuta wanalipa dola mia 600
zaidi kwa ajili ya dawa na matibabu na gharama nyenginezo. Na watu
watakaofaidika kutokana na kufutiliwa mpango huo ni makampuni ya bima.”
alisema Obama.
Mbali na hayo Obama na Romney walizungumzia maoni yao juu ya jukumu
la serikali kuu. Obama akisema kuna tofauti kati yao yeye akiamini
jukumu la kwanza la serikali ni kuwalinda wananchi, pili kuwapatia
elimu, hivyo anataka kuajiri walimu zaidi hasa wa sayansi na teknolojia
ili Marekani iweze kuongeza tenakatika fani hizo.
Romney anasema inabidi watu binafsi wawajibike na kuacha majimbo kuongoza katika elimu.
Wachambuzi wamegawika juu ya nani aliyeshinda kinyume na wapiga kura waloamua kwamba Romney anmeshinda.
Category:
0 comments