machafuko yatanda Zanzibar

Unknown | Friday, October 19, 2012 | 0 comments


Taarifa kutoka visiwani Zanzibar nchini Tanzania zinasema kuwa, hali ya usalama visiwani humo bado sio shwari kufuatia kutoweka katika hali ya kutatanisha kiongozi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Uamasho Sheikh Farid Hadi Ahmed. Hali ya taharuki na machafuko ilianza kushuhudiwa katika maeneo ya mkoa wa Mjini Magharibi kisiwani Ungauja hapo jana baada kuenea taarifa za kukamtawa na kutekwa nyara na watu wasiojulikana Sheikh Farid ambaye pia ni msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa askari mmoja wa kikosi cha kutuliza ghasia cha FFU ameuawa kwa kupigwa mapanga na kukatwa kichwa na watu wasiojulikana huku kukishuhudiwa pia vitendo kadhaa vya uhalifu ikiwa ni pamoja na kuchomwa moto nyumba za wageni, maskani ya CCM ya Kisonge mjini Unguja, maeneo ya biashara na hata mali za wananchi. Katika hali ambayo vyombo vya usalama vinayahusisha matukio hayo na wafuasi wa Uamsho, Katibu wa jumuiya hiyo Sheikh Abdullah Said amekanusha tuhuma hizo na kusema kwamba wafuasi wa taasisi hiyo ya Kiislamu hawahusiki na vitendo hivyo. Taarifa zaidi zinasema kuwa, machafuko hayo yanashuhudiwa zaidi katika maeneo ya Darajani, Michenzani, Muembeladu, Magomeni na Amani. Wakati huo huo Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa amesema kuwa, Sheikh Farid amepotea katika hali ya kutatanisha, na kwamba hadi sasa juhudi za kumtafuta bado zinaendelea.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments